Raia wa Croatia wamekamatwa tena nchini Zambia kwa tuhuma za ulanguzi (kuiba/kusafirisha watoto).
Wiki chache zilizopita raia hao waliachiwa huru baada ya mahakama kutupilia mbali mashitaka hayo, lakini wiki hii siku ya alhamisi tarehe 9 walikamatwa tena wakiwa katika hatua za kurudi nchini kwao.
Hivi sasa raia hao ambao ni wanandoa wanashitumiwa tena kwa kudaiwa kusafirisha watoto kutoka nchi ya Congo na Zambia.
Aidha washitakiwa hao walitoa utetezi wao kuwa walifuata taratibu zote za nchi hiyo juu ya kuasi watoto hao wakiongozwa na wakili wao.
Comments