![](https://static.wixstatic.com/media/84f169_9d82bd2328bf4188b06558acbbec1e71~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_653,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/84f169_9d82bd2328bf4188b06558acbbec1e71~mv2.jpg)
MKE wa marehemu Augustine Mrema, mwanasisasa mashuhuri nchini aliyefariki dunia 21 Agosti na kuzik wa juzi Alahmisi, Doreen Kimbi Mrema, ameanza kuonja joto ya jiwe kutoka kwa familia ya kiongozi huyo mara baada ya ndugu hao kupinga wosia ulioachwa na marehemu kuhusu ugawaji wa mali.
Sakata hili liliibuka siku chache tu takribani siku tano baada ya mazishi ya mzee Mrema ambapo familia ilianza kupinga ugawaji wa mirathi hiyo kwa kuanza na kugoma kumuachia aliyekua mke wa mzee Mrema (Doreen Mrema) nyumba iliyoko Mbezi salasala na kuzuia matumizi ya gari iliyokuwa inatumiwa na marehemu mzee Mrema.
![](https://static.wixstatic.com/media/84f169_ddf492b279104e109826a037bd556105~mv2.jpg/v1/fill/w_720,h_433,al_c,q_80,enc_avif,quality_auto/84f169_ddf492b279104e109826a037bd556105~mv2.jpg)
Ndugu hao wa familia waliendelea kusisitiza kuwa mke huyo hastahili kupata mali licha ya kuwepo kwa wosia ulioachwa ukihitaji yeye apatiwe sehemu ya urithi wa aliyekua mumewe.
Jambo hili lilitekelezwa kwa gari hiyo kutolewa matairi yote manne ili isiweze kutumika.
Ikumbukwe k uwa siku chache kabla ya maziko katika ibada ya mazishi, kiongozi wa dini Padri Deogratius Mashika alisihi familia hiyo kuepukana na migogoro kuhusu mirathi. Maneno hayo ya Padri Mashika hayakuleta tija yoyote kwani hadi kufikia leo sakata hili limefikia hali mbaya ambapo kumekua na mgogoro mkubwa kuhusu wosia.
Commentaires