top of page

Panya road wavamia na kuua

Daniel Dos santos

Kundi la kihalifu maarufu kama panya road limeibuka upya tena baada ya kuvamia, kujeruhi na kuua mmoja hapa Kawe Dar es salaam.



Kamanda wa polissi kanda maalum, William Monda ameijulisha jamii kuwa aliyeuawa ni mwanafunzi aliyekua akisoma mwaka wa pilli katika chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM)

Inasadikika kuwa tukio hilo lilifanywa na kikundi cha vijana wanaokadiriwa kuwa kumi huku wakiwa na silaha za jadi ambapo walivamia nyumbani kwa marehemu eneo la Kawe.

Jeshi la polisi limethibitisha kukamatwa kwa baadhi ya vijana kutoka katika kundi hilo na kuahidi kuendelea kuwasaka na kuwatia katika mkono wa sheria.

Aidha, Kamanda wa polisi ametoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kufichua uhalifu wa aina hiyo.

6 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page