top of page

KUTOKA KAMBI YA WAKIMBIZI HADI KUCHEZA WORLD CUP

Daniel Dos santos


Wenzetu wazungu wanasema "Dreams do come true" wakimaanisha Ndoto hutimia.

Kama wewe ni mpenzi wa soka jina la Alphonso Davies haliwezi kuwa jina geni kwako. Huyu ni mchezaji anayekipiga katika timu ya Bayern Munchen ya Ujerumani.

Historia ya mchezaji huyu mahiri ambaye kwa mara ya kwanza anaenda kucheza kombe la dunia akiwa katika timu ya taifa ya Canada imevutia watu wengi na kuwapelekea watu kuamini kuwa hakuna kinachoshindikana endapo mtu ataweka nia ikiwemo pamoja na kumwamini Mungu.

Hii hapa chini ni historia fupi ya kijana huyu beki safi kabisa ya Bayern Munchen


- Utaifa : Wazazi wake ni raia wa nchi ya Liberia ambao walikimbilia nchini Ghana kwenye kambi ya wakimbizi sehemu ambapo star huyu wa Bayern Munchen alizaliwa.


- Utaifa wa sasa : Tarehe 6/6/2017 Alphonso Davies alifanikiwa kupata uraia wa Canada na hadi leo ni mmoja kati ya wachezaji tegemezi wa timu hiyo inayoshiriki mashindano ya kombe la dunia yatakayoanza hivi karibuni.



19 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page