top of page

Je unajua kuwa sheria inaruhusu mama kutomwambia mtoto nani ni baba yake halisi?

Daniel Dos santos

Kulingana na shauri la Kuruthum Omary Kahiba and Another vs Mwajuma Omary Kahiba (Misc. Civil Cause 4 of 2018) [2020] TZHC 3597 (29



Watoto walimshitaki mama yao ili awaambie baba yao halisi na kuiomba mahakama imlazimishe mama yao kuwaambia baba yao halisi ni nani? Maana wamekuwa wakiishi toka utotoni hawamjui baba yao halisi na wana haki ya kujua hivyo walituma maombi mahakamani kuamuru/ shinikiza mama yao awaambie baba yao halisi. Jaji aliwajibu kuwa mama anaweza kuwa baba kwa maana anaweza kuwalea pekee yake bila baba hivyo hakuna umuhimu wa kulazimishwa kueleza watoto baba yao halisi ni nani. Na alieza sababu zifuatazo 1.Huenda hajui tofauti ya baba mzazi wa mtoto kwa sababu alishiriki ngono na wapenzi wengi karibu na wakati wa mimba ya mtoto. 2. Hakumbuki ni nani alijamiiana nae wakati wa mimba ya mtoto. Hivyo ngumu kuwa na majibu sahihi 3. Mtoto anaweza kua alipatikana kwa njia ya kupandikiza mbegu za mwanaume ambapo hamjui au hataki kumtaja, au hajafuatilia historia ya aliyettoa hizo mbegu za uzazi. Hili hufanyika hasa kwa wenzetu wa ulaya.


4. Mtoto anaweza kuwa ni matokeo ya tukio la ubakaji ambao mama anataka ibaki kuwa faragha. Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa mama ni mwathirika wa unyanyasaji wa kingono, anaweza kuogopa kuteswa na mume wake, na baba mzazi wa mtoto wake, au kutoka kwa mnyanyasaji mwingine. anafichua utambulisho wa baba mzazi wa mtoto wake. 5. Mtoto anaweza kuwa matokeo ya uhusiano wa nje ya ndoa ambayo mama hataki kufichua na anataka iwe siri yake. Natumaini umeelimika vyya kutosha kuhusu makala hii. Usisite kuniuliza maswali au kuchangia maoni yako juu yaa sheria hii.


4 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page